AMMAN: Misaada kwa wakimbizi wa Kiiraki | Habari za Ulimwengu | DW | 27.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

AMMAN: Misaada kwa wakimbizi wa Kiiraki

Mkutano wa kimataifa kuhusu miradi ya misaada kwa wakimbizi wa Kiiraki wapatao kama milioni 2.2 umemalizika mji mkuu wa Jordan,Amman.Ujumbe wa Syria umezitaka Marekani na Irak zichangie zaidi kulitenzua tatizo hilo la wakimbizi.

Katibu wa taifa katika wizara ya mambo ya ndani ya Jordan,Mukhaibar Abu Shamus amesema, serikali ya Jordan sasa itawaruhusu wanafunzi wa Kiiraki kwenda katika shule za serikali na za binafsi.Vile vile wakimbizi wa Kiiraki wataruhusiwa kutumia hospitali za serikali na Jordan italipa ruzuku ya asilimia 65 kwa huduma hizo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com