ALGIERS:Watu 15 wameuwawa kwenye shambulio la bomu | Habari za Ulimwengu | DW | 07.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ALGIERS:Watu 15 wameuwawa kwenye shambulio la bomu

Takariban watu 15 wameuwawa wakati mshambuliaji wa kujitoa muhanga alipojilipua kwa bomu katika eneo la Batna mashariki mwa Algeria.

Watu 70 wamejeruhiwa kwenye shambulio hilo wakati walipokuwa wanamsubiri rais Abdulaziz Bouteflika aliyekuwa anatarajiwa kuzuru eneo hilo.

Rais Bouteflika baadae alitoa hotuba katika televisheni ya taifa aliilaani shambulio hilo na amesisitiza kuwa ataendeleza juhudi zake za kusaka maridhiano ya kiaifa ambayo yanatoa fursa ya msamaha kwa vikundi vyenye itikadi kali na ambavyo vitakuwa tayari kuacha vitendo vya mashambulio.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com