AL FASHER:Katibu mkuu azuru jimbo la Darfur | Habari za Ulimwengu | DW | 05.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

AL FASHER:Katibu mkuu azuru jimbo la Darfur

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon ambae leo anazuru jimbo la Darfur nchini Sudan amesema jamii ya kimataifa haikuwajibika vya kutosha ili kumaliza mapigano ya miaka minne katika jimbo la Darfur.

Ziara ya katibu mkuu wa umoja wa mataifa nchini Sudan inalenga kufufua tena mazungumzo ya amani ya jimbo la Darfur kabla kupelekwa majeshi ya kulinda amani ya umoja wa mataifa kwa ushirikiano na vikosi vya jeshi na polisi vya umoja wa Afrika katika eneo la Al Fasher kaskazini mwa jimbo la Darfur.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amefhamisha kwamba maelezo kamili yanashughulikiwa juu ya mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Khartoum na makundi ya waasi ambayo hayakutia saini mkataba wa amani wa mwezi Mei mwaka 2006.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com