ADDIS ABABA.Serikali yawafuta kazi maafisa wake watatu wa ngazi za juu | Habari za Ulimwengu | DW | 20.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ADDIS ABABA.Serikali yawafuta kazi maafisa wake watatu wa ngazi za juu

Serikali ya Ethiopia imewafuta kazi maafisa wake watatu wa ngazi za juu katika jeshi la nchi hiyo.

Msemaji wa wizara ya ulinzi wa Ethiopia Dawit Assefa amesema kwamba maafisa hao ni meja generali Almeshet Degfe wa kikosi cha wanahewa, brigadia jenerali Kumeri Assefa wa jeshi la Ethiopia na Asamenew Tsgie wamepigwa marufuku kujihusisha na shughuli za ulinzi wa nchi hiyo.

Hata hivyo msemaji wa wizara ya ulinzi amesema hana taarifa zaidi juu ya uamuzi huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com