1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Abiy Ahmed Ali

Abiy Ahmed Ali ndiye mwenyekiti mpya wa muungano tawala nchini Ethiopia wa EPRDF na chama cha kabila la Oromiya cha OPDO, ambacho ni mmoja ya vyama vinne vinavounda muungano wa EPRDF.

Abiy pia ni mbunge aliechaguliwa na mjumbe wa kamati ya uongozi ya EPRDF. Hadi 2018 alihudumu kama mkuu wa sekriteriat ya OPDO na ofisi ya maendeleo ya makaazi na mji wa Oromiya akiwa na cheo cha Naibu rais wa jimbo la Oromiya, mmoja ya majimbo tisa ya Ethiopia. Abiy Ahmed alizaliwa August 15, 1976 nchini Ethiopia. Alikulia katika familia ya lugha na dini tofauti, ambapo baba yake Ahmed Ali ni Muislamu na mama yake ni Mkristo. Katika ukurasa huu utakuta maudhui za DW kuhusu Abiy Ahmed.

Onesha makala zaidi