ADDIS ABABA: Waandishi 25 wa habari waachiliwa huru | Habari za Ulimwengu | DW | 10.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ADDIS ABABA: Waandishi 25 wa habari waachiliwa huru

Jaji mmoja nchini Ethiopia amewaachilia huru waandishi 25 wa habari na wapinzani wa serikali. Washukiwa hao walikabiliwa na vifungo vya maisha gerezani au hukumu ya kifo kwa mashtaka ya uhaini na jaribio la kufanya mauaji ya halaiki.

Jaji huyo pia ameyafutulia mbali mashataka kama hayo dhidi ya viongozi zaidi ya 130 wa upinzani, wafanyakazi wa kutoa misaada ya kiutu na wanachama wa vyama vya wafanyakazi, akisema waendesha mashtaka walishindwa kutoa ushahidi.

Hata hivyo bado wanakabiliwa na mashtaka mengine ikiwa ni pamoja na jaribio la kutaka kuipindua serikali.

Kesi hiyo ilisababishwa na visa viwili vya kuzuka machafuko baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2005 ambapo watu takriban 80 waliuwawa.

Kesi hiyo imekosolewa na jamii ya kimataifa kwa kuchochewa kisiasa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com