ADDIS ABABA: Mpango mpya wa usuluhishi wa mgogoro wa Darfur-Sudan | Habari za Ulimwengu | DW | 17.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ADDIS ABABA: Mpango mpya wa usuluhishi wa mgogoro wa Darfur-Sudan

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan, ametoa msukumo mpya kuelekea suluhisho la mzozo wa eneo lenye machafuko la Darfur, magharibi mwa Sudan.

Mpango mpya wa Umoja wa mataifa unasema papelekwe katika jimbo hilo la Darfur kikosi cha kijeshi cha kulinda amani chenye mchanganyiko wa wanajeshi 20,000 wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika. Akizungumza baada ya kumalizika mazungumzo kati ya Umoja wa mataifa, Umoja wa Afrika na serikali ya Sudan mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, Kofi Annan amesema Sudan imekubali kimsingi pendekezo hilo lakini hawajakubaliana kuhusu idadi ya wanajeshi watakaopelekwa huko. Serikali ya Sudan ilisema ina wasi wasi pia kuhusu nani atakaoongoza kikosi hicho cha kijeshi cha kimataifa.

Muda wa kikosi cha wanajeshi wa kulinda amani kutoka nchi za kiafrika unamalizika mwishoni mwa mwaka huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com