4 wauwa kwa bomu la kutegwa Sri Lanka | Habari za Ulimwengu | DW | 02.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

4 wauwa kwa bomu la kutegwa Sri Lanka

COLOMBO:

Bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara limelipuka karibu na bas lililokuwa limewabeba wanajeshi katika mji mkuu wa Sri Lanka wa Colombo.

Watu wanne wameuawa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa.Maafisa wa jeshi wanawalaumu waasi wa Kitamil kwa shambulio hilo. Mlipuko huo ni mmoja wa mashambulizi mapya dhidi ya vituo vya kijeshi.Shambulio la sasa limekuja baada ya mapigano mapya kati ya majeshi ya serikali na waasi katika eneo la kaskazini la nchi hiyo.Vita vya nchini Sri Lanka vimesababisha watu wapatao elf 30 kupoteza maisha yao tangu mwaka wa 1983.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com