Wito kuidhinisha upesi Mkataba wa Mageuzi wa Umoja wa Ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 14.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wito kuidhinisha upesi Mkataba wa Mageuzi wa Umoja wa Ulaya

LISBON: Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya,Jose Manuel Barroso amezihimiza nchi 27 wanachama katika umoja huo,kuidhinisha upesi Mkataba wa Mageuzi wa Umoja wa Ulaya uliotiwa saini mjini Lisbon. Kuambatana na mpango wa Barroso,mkataba huo uanze kutumika tarehe 1 Januari mwaka 2009.

Mkataba huo unatazamiwa kufungua ukurasa mpya katika historia ya Umoja wa Ulaya na kuimarisha demokrasia katika utaratibu wa kupitisha maamuzi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com