Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani ziarani kanda ya Balkan | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 26.08.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani ziarani kanda ya Balkan

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle hii leo anaendelea na ziara yake katika kanda ya Balkan kwa kuzitembelea Serbia na Bosnia.

Außenminister Guido Westerwelle (FDP) spricht am Mittwoch (25.08.2010) auf dem Flug nach Zagreb mit Journalisten. Westerwelle ist zu einer dreitägigen Balkan-Reise aufgebrochen. Foto: Hannibal dpa/lbn +++(c) dpa - Bildfunk+++

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Guido Westerwelle.

Mada kuu ya majadiliano yake katika mji mkuu wa Serbia Belgrade,ni mgogoro unaohusika na suala la kuutambua uhuru wa Kosovo.

Majadiliano yanayohusika na uanachama wa Serbia katika Umoja wa Ulaya, hayakufanikiwa mpaka hivi sasa kwa sababu ya nchi hiyo kukataa kutambua uhuru wa Bosnia. Hii leo mjini Belgrade, waziri Westerwelle atakutana na Rais Boris Tadic na maafisa wengine wa Serbia.

Westerwelle alianzia ziara yake nchini Croatia na aliarifu kuwa nchi hiyo inakaribia kukamilisha utaratibu wa kuingia katika Umoja wa Ulaya.

Mhariri: P.Martin/ZPR

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com