1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yellen ahimiza mipango kabambe kwa mali za Urusi

24 Mei 2024

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen amewahimiza mawaziri wenzake kutoka mataifa ya G7 wanaokutana nchini Italia, kuzingatia njia bora zaidi za kutumia mali za Urusi zilizozuwiwa kuisadia Ukraine.

https://p.dw.com/p/4gDYU
Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen,
Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen,Picha: Johannes Neudecker/dpa/picture alliance

Mawaziri na magavana wa benki kuu kutoka mataifa ya G7 wanakutana mjini Stresa, Italia, kuandaa mkutano wa kilele wa viongozi wakuu wa mataifa na serikali mjini Puglia mwezi ujao.

Yellen amasema kundi hilo litajadili kile Washington inakizingatia kuwa "uwezo kupita kiasi" wa teknolojia za kijani kutoka China, kama vile magari ya umeme, betri na paneli za umeme wa jua.

Soma pia: Yellen: Marekani haitakubali viwanda kuharibiwa na China

Juu kwenye ajenda ya mkutano huo ni mpango wa ufadhili wa Ukraine kwa kutumia riba iliyotokana na kiasi cha euro bilioni 300 za mali za benki kuu ya Urusi, zilizozuwiwa na G7 na Ulaya.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, anatazamiwa kuhudhuria mkutano wa wakuu wa G7 pia, kulingana na ripoti za gazeti la Bloomberg.