1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yellen: Marekani haitakubali viwanda kuharibiwa na China

8 Aprili 2024

Waziri wa Fedha wa Marekani Janeth yellen amesema, Marekani haitokubali viwanda vipya kuharibiwa na bidhaa za ruzuku kutoka China, bidhaa mabzo zinatajwa kutishia soko la kimataifa kwa mataifa mengine

https://p.dw.com/p/4eYTF
China, Beijing | US Janet Yellen
Waziri wa Fedha wa Mrekani, Janeth YellenPicha: Tatan Syuflana/AP/picture alliance

    

Waziri wa Fedha wa Marekani Janeth yellen amesema Marekani haitokubali viwanda vipya kuharibiwa na bidhaa za ruzuku kutoka China. Waziri huyo amayasema hayo wakati akimaliza mkutano wa siku nne wa kuishinikiza China kudhibiti uwezo wake wa utengenezaji  bidhaa za viwandani mjini Beijing.

Soma zaidi. Yellen asema Marekani haitakubali viwanda vipya kuharibiwa na bidhaa za bei nafuu kutoka China

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, waziri wa fedha wa Marekani amesema Rais Joe Biden hawezi kuruhusu kutokea kwa mambo yaliyotokea mwanzoni mwa miaka ya 2000 wakati China ilipoingiza bidhaa nyingi nchini marekani na kuharibu kazi za uzalishaji karibu milioni mbili za wamarekani.

China, Beijing | Li Qiang / Janet Yellen
Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen ameizuru China kwenda kulalamika juu ya uwekezaji mkubwa wa kiviwanda unaofanywa na China Picha: Tatan Syuflana/Pool/REUTERS

Soma zaidi. Yellen asema mahusiano ya Marekani na China yanaimarika lakini bado kuna mengi ya kufanya

Lakini pamoja na hayo Janeth Yellen hakutishia kuweka viwango vipya vya ushuru kwa biashara za China na kwamba Beijing iendelee na mpango wake wa kuzalisha magari ya umeme, betri za umeme wa jua na bidhaa nyingine za nishati.

Yellen: Marekani na China zinategemeana

Yellen ameizuru China kwa mara ya pili baada ya miezi tisa kwenda kulalamika juu ya uwekezaji mkubwa wa kiviwanda unaofanywa na China na ambao unazidi mahitaji ya ndani, kitendo ambacho Marekani na mataifa mengine yanaona kama ni kitisho kwenye soko la kimataifa.

China, Beijing | Li Qiang /Janet Yellen
Waziri wa fedha wa Marekani amehitimisha mkutano wake wa siku nne wa kuishinikiza China kudhibiti uwezo wake wa utengenezaji  bidhaa za viwandani mjini Beijing.Picha: Tatan Syuflana/Pool/REUTERS

"Wakati wa mazungumzo wiki hii, nilisisitiza tena kwamba Marekani haina mpango wa kusitisha kabisa mahusiano na China. Uchumi wa nchi hizi mbili unategemeana sana, na kusitisha uhusiano itaathiri uchumi wa kwetu sisi wawili.  Hata tunapochukua hatua za kubadilishana,  njia za usambazaji  na  tunatafuta kujenga uhusiano mpana wa biashara na uwekezaji ambao unaweza kuwanufaisha wafanyakazi na makampuni ya Marekani. China ni soko kuu la bidhaa na huduma za Marekani, Na ushindani kati ya makampuni yetu unaweza kuchochea nguvu zaidi na uvumbuzi katika sekta ya viwanda Marekani´´ amesema Janeth Yellen.

Kwa upande mwingine, Bunge la China lilisema mwezi Machi kuwa litachukua hatua za kupunguza uzalishaji mkubwa wa viwanda nchini humo.

Soma zaidi. China yakanusha tuhuma za ruzuku za magari ya umeme

Lakini hapa karibuni pia Beijing ilijibu mapigo kwa Marekani na mataifa mengine ya Ulaya juu ya uwezo wake wa kuzalisha bidhaa na ulikuwa unatishia uwezo wa mataifa mengine katika soko la kimataifa ulikuwa umepotishwa

Itakumbukwa kuwa, Waziri wa Biashara wa China Wang Wentao alipinga wazi wazi madai ya ongezeko la magari ya umeme yanayotengenezwa na China katika mkutano uliofanyika mjini Paris na kusema kwamba hayana mashiko.