Waziri mkuu wa Zimbabwe ziarani Ujerumani | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.06.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Waziri mkuu wa Zimbabwe ziarani Ujerumani

Ujerumani yaahidi misaada zaidi ya kiutu kwa sharti demokrasia inaimarishwa

Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgen Tsvangirai

Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgen Tsvangirai

Waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgen Tsvangirai, akiwa ziarani nchini Ujerumani, ameitolea mwito jumuia ya kimataifa izidi kuisaidia nchini yake. Bwana Morgen Tsvangirai, anaefanya ziara ya wiki tatu katika miji mikuu ya nchi za Magharibi,alikua na mazungumzo pamoja na kansela Angela Merkel mjini Berlin hii leo.

Kansela Angela Merkel amemhakikishia waziri mkuu Morgen Tsvangirai kwamba Ujerumani itazidisha msaada wake kwa Zimbabwe. Katika mazungumzo yao katika ofisi ya kansela mjini B erlin, kansela Angela Merkel aliyemtaja waziri mkuu Tsvangirai kua ni "kitambulisho cha utaratibu wa kuleta demokrasia nchini Zimbabwe", amefungamanisha misaada zaidi ya kiutu na kuimarishwa utaratibu wa kidemokrasi nchini Zimbabwe. Kansela Angela Merkel amekiri katika kipindi cha miezi iliyopita kuna "mambo yaliyoanza kuchomoza," ughali wa maisha umeanza kupungua na shule zimefunguliwa, amesema. Hata hivyo, kansela Angela Merkel hakutaja kiwango cha misaada Ujerumani inayopanga kuipatia Zimbabwe.

Kansela Angela Merkel ameahidi kuyahimiza makampuni ya Ujerumani yawekez e nchini Zimbabwe.

Waziri mkuu huyo wa Zimbabwe anaefanya ziara ya wiki tatu katika miji mikuu ya dunia ili kujaribu kurejesha imani ya walimwengu iliyochafuliwa na utawala wa rais Robert Mugabe, ameahidi nchi yake itajirekebisha. "Nchi yake imetaabika vya kutosha kiuchumi kufuatia miaka zaidi ya kiumi ya kutengwa", amesema waziri mkuu Tsvangirai, na kuahidi "Zimbabwe haitorejea tena katika enzi za kale na vitisho."

Waziri mkuu wa Zimbabwe alikutana pia na waziri wa mambo ya nchi za nje ,Frank-Walter Steinemeier.Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nchi za nje mjini Berlin, makamo kansela ameitaka serikali ya Zimbabwe izidishe juhudi za kuimarisha demokrasi. Amezisifu hatua za serikali ya mpito za kupiga vita kipindu pindu na kupunguza ughali uliokithiri wa maisha. Waziri wa mambo ya nchi za nje amezungumzia umuhimu wa kuimarishwa usalama nchini Zimbabwe. "Ujerumani iko tayari kushirikiana na Zimbabwe ya kidemokrasi ijikwamue na kurejea katika jumuia ya kimataifa", amesema waziri wa mambo ya nchi za nje Frank-Walter Steinmeier.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Othman Miraji

 • Tarehe 15.06.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/IAG1
 • Tarehe 15.06.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/IAG1
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com