Waziri mkuu wa Thailand aazimia kuendeleza makabiliano dhidi ya waandamanaji. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 15.05.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Waziri mkuu wa Thailand aazimia kuendeleza makabiliano dhidi ya waandamanaji.

Watu 22 wauawa katika makabiliano nchini Thailand, 194 wajeruhiwa.

default

Mji wa Bangkok, Thailand wabadilika na kuwa uwanja wa vita.

Waziri mkuu wa Thailand, Abhisit Vejjajiva amesema serikali haitarudi nyuma katika jitihada za kukabiliana na waandamanaji aliowataja kama wanaovunja sheria na kuunda makundi ya wapiganaji wanaojaribu kutisha serikali.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki Moon ametoa wito wa kusitishwa kwa ghasia katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok huku wanajeshi na waandamanaji wanaoipinga serikali wakiendelea kukabiliana .

Wanaotoa huduma za dharura nchini humo wamesema kuwa idadi ya watu waliouawa imefikia 22 na wengine zaidi ya 194 wamejeruhiwa .

Ban ki Moon amewahimiza viongozi wa serikali na waandamanaji wanaovaa mashati mekundu warejee kwenye mazungumzo.

Thailand Bangkok Demonstrationen No-Flash

Waziri mkuu wa Thailand asema waandamanaji wanavunja sheria na wanajaribu kuitisha serikali.

Vikosi vya wanajeshi vimeshiriki katika makabiliano makali ya siku mbili na waandamanaji ambao walivurumisha mawe na mabomu ya petroli baada ya wanajeshi kuingia katika eneo la kibiashara la Rath-Chap-Rasong.

Wanajeshi hao waliingia katika enelo hilo kwa lengo la kuukomesha mvutano ambao sasa umeingia katika mwezi wa pili baina ya waandamanaji na serikali ya waziri mkuu, Abhisit Vejjajiva.

Mwandhishi, Peter Moss /Reuters

Mhariri, Abdu Mtullya

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com