Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu asisitiza kuwa Jerusalem utasalia kuwa mji mkuu wa Israel. | Matukio ya Kisiasa | DW | 22.05.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu asisitiza kuwa Jerusalem utasalia kuwa mji mkuu wa Israel.

Palestina inataka eneo la mashariki mwa mji wa Jerusalem kuwa mji wake mkuu, wakati taifa la Palestina litakapoundwa.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa hii leo kuwa mji wa Jerusalem utasalia kuwa mji wa Israel milele huku Israel ikiadhimisha miaka arobaini na mbili baada ya kulichukua kwa nguvu eneo la mashariki la mji huo lenye wakaazi wengi wa kiarabu.

Jerusalem ni mji mkuu wa Israel, umekuwa tangu hapo na utasalia hivyo milele, na kamwe hautagawanwa, alisema waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wakati wa sherehe za kuadhimisha kuchukuliwa kwa nguvu eneo lililo mashariki mwa Jerusalem, wakati wa vita vya siku sita vilivyo piganwa mwaka 1967.

Jamii ya kimataifa haiutambui mji wa Jerusam kama mji mkuu wa Israel na suala hili linaonekana kama kizingiti kwa mchakato wa amani kati ya Israel na Palestina inayotaka eneo la mashariki mwa Jerusalem kuwa mj wao mkuu baada ya kuundwa kwa taifa la Palestina.

Maelfu ya watu, wengi wao wakipeperusha bendera walijipanga katika mji wa Jerusalem wakati ambapo karibu wapalestina 200 pamoja na wanaharakati wa mrengo wa kushoto wa Israel walifanya maandamano katika mji wa zamani wa Damascus.

Uhusiano wa wayahudiu na mji wa Jerusalem ni wa tangu wa maelfu ya miaka iliyopita na mjii huu utasalia chini ya taifa letu,“ alisema Netanyahu katika mlima wa Ammunition kulikofanyika mapigano makali kati ya wanajeshi wa Israel na wa Jordan mwezi Juni mwaka 1967.

Maadhimisho hayo yanafanyika kila mwaka kuambatana na kalenda ya kiyahudi.

Palästinenserpräsident Mahmud Abbas in seinem Büro

Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas.

Msemaji wa rais wa mamlaka ya palestina mahamoud Abbas, alisema kuwa eneo la mashariki mwa Mji wa Jerusalem linakaliwa la wapalestina kama vile Waisraeli wanavyoyakalia maeneo ya Palestina tangu Juni nne mwaka 1967.

Nabil Abu Rudeina alisema kuwa matamshi kama hayo yanavuruga mpango wa kuundwa kwa mataifa mawili na kumwomba rais wa Marekani Barack Obama kuingilia kati ili kukomesha sera za Israel, zinazohujumu juhudi za kupatikana kwa amani katika eneo hilo.

Siku ya Alhamisi wabunge wa Israel kutoka upande wa mrengo wa kulia unaotawala, waliwasilisha mswada bungeni ulio na lengo la kuzuia kugawanwa mwa mji wa Jerusalem kwa Wapalestna.

Mswada huo utahitaji mabadilo yoyote yatakayofanyiwa mipaka ya Jerusalem kupata uungwaji mkono wa asilimia 80 miongoni mwa wabunge mia na ishirini kinyume na asilimia sitini na moja iliyopo sasa.

Seriali iliyotanguliwa ilikuwa imeonyesha ishara kuwa Israel, huenda ikasalimisha eneo la masahariki mwa mji wa Jerusalam kwa waarabu.Hata hivyo serikali ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu iliyoingia madarakani tarehe 31 mwezi machi mwaka huu, imelipinga suala hilo na hivyo kupata lawama kali za kimataifa kwa kuzuia kuidhinisha kuundwa kwa taifa la Palestina.

Sasa hivi mji wa Jerusalem una karibu wakazi 760,000 wakiwemo wayahudi 492,400 na waarabu 268,400. kati ya hawa asilimia 74 ya watoto wa kiarabu wanaishi katika hali ya umaskini ikilinganishwa na asilimia 48 ya watoto wa kisrael.

Katika upande mwingine raia wawili wa kipalestina waliuawa mapema hii leo katika eneo la ukanda wa Gaza. Jeshi la Israel lilisema kuwa wanaume hao waliokuwa wamejihaki walipigwa risasi wakati walikuwa wakifanya jaribio la kutega bomu kwenye kizuizi.

Mwandishi :Jason Mogaka Nyakundi/AFP

Mhariri : Mohammed Abdul Rahmam


Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com