Waziri Kouchner wa Ufaransa kukutana na viongozi wa Libanon | Habari za Ulimwengu | DW | 04.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Waziri Kouchner wa Ufaransa kukutana na viongozi wa Libanon

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa,Bernard Kouchner hii leo amerejea Libanon kujadiliana na viongozi wanaohasimiana kuhusu wadhifa wa rais. Ofisi ya Waziri Mkuu wa Libanon Fouad Siniora imesema,Kouchner atakutana na Siniora.Wakati huo huo kituo cha televisheni cha Libanon kimesema, Kouchner atakutana na viongozi wa serikali inayodhibitiwa na wanasiasa wanaoungwa mkono na mataifa ya Magharibi na pia wapinzani wanaoungwa mkono na Hezbollah.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com