Wauguzi watano wa Bulgaria na daktari mmoja wa Palastina huuenda wakatolewa jela hivi karibuni | Habari za Ulimwengu | DW | 27.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wauguzi watano wa Bulgaria na daktari mmoja wa Palastina huuenda wakatolewa jela hivi karibuni

Tripoli

Korti moja nchini Libya imeamuru waachiwe huru wauguzi watano wa Bulgaria na daktari mmoja wa kiipalastina waliokua wakishikiliwa kwa tuhuma za “kusema uwongo”mbele ya polisi wanaodai wamewatesa walipokua wakiwahoji katika kesi iliyopelekea kuhukumiwa adhabu ya kifo.Katika kesi hiyo iliyodumu chini ya dakika moja hii leo,jaji Salem al Homari ametangaza kuachiwa huru wauguzi hao watano wa Bulgaria na daktari mmoja wa kipalastina.Gharama za mahakama zitalipwa na polisi.Watuhumiwa hao sita walihukumiwa adhabu ya kifo mwezi May mwaka 2004 kwa makosa ya kuwaambukiza makusudi virusi vya UKIMWI watoto katika hospitali ya Benghazi kaskazini mashariki ya Libya.Hukmu hiyo ilithibitishwa tena mwezi December mwaka jana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com