1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Watu watatu wauawa baada ya Urusi kushambulia mji wa Odesa

6 Aprili 2026

Mashambulizi ya Urusi Kusini mwa mji wa Odesa nchini Ukraine yamewaua watu watatu akiwemo mtoto wa miaka miwili na kusababisha pia umeme kukatika mjini humo.

https://p.dw.com/p/5Bjqm
Ukraine Odessa 2026 | Brand in Wohngebäude nach russischem Angriff
Urusi yashambulia mji wa Odesa na kusababisha mauaji ya watu watatu akiwemo mtoto wa miaka miwiliPicha: State Emergency Service of Ukraine/AFP

Kampuni kubwa kabisa ya kibinafsi ya nishati nchini Ukraine, DTEK, imesema zaidi ya watu 16,000 wameachwa bila umeme kufuatia shambulizi hilo.

Moscow imekuwa ikiishambulia Ukraine masaa ya usiku ndani ya miaka yake minne tangu ilipoanza uvamizi wake wa kijeshi dhidi ya jirani yake na kuanzisha mgogoro mkubwa barani Ulaya ambao haujawahi kushuhudiwa  tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia.

Rais wa Ukraine  Volodymyr Zelensky ametoa salamu zake za pole kwa familia za waliouwawa huku akiongeza kuwawatu wengine 16 wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo.

Zelensky ameongeza kuwa Urusi ilirusha droni zaidi ya 140 zilizoharibu pia maeneo yake ya nishati ya miji ya Chernihiv, Sumy, Kharkiv, na Dnipro.