WASHINGTON:Kundi la kijeshi la Iran Revolutionary Guard kuorodheshwa na magaidi | Habari za Ulimwengu | DW | 15.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Kundi la kijeshi la Iran Revolutionary Guard kuorodheshwa na magaidi

Marekani inapanga kulitangaza kundi la Iran Revolutionary Guard kuwa kundi la Kigaidi.Hatua hiyo inalenga kusambaratisha mtandao wa kibiashara wa kitengo cha kijeshi cha kundi hilo.Kwa mujibu wa afisa mmoja wa serikali ambaye hakutaka kufahamika Rais George Bush anapanga kutoa agizo litakalofanikisha juhudi za kuwezesha serikali kuzuia mali za kundi hilo.

Marekani inashuku kuwa kundi hilo lililo na wanachama laki moja ishirini na tano linaunga mkono vitendo vya ugaidi nchini Iraq,Afghanistan na eneo la mashariki ya kati kwa jumla.

Agizo hilo huenda likatolewa katika kipindi cha siku chache zijazo.Endapo agizo hilo linatekelezwa Kundi la kijeshi la Revolutionary Guard litakuwa la kwanza kuorodheshwa pamoja na watu binafsi,mashirika ya misaada na makundi yanayoaminika kuwa ya kigaidi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com