WASHINGTON:Bunge la Congress lasubiri tathmini ya Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 12.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Bunge la Congress lasubiri tathmini ya Iraq

Bunge la Marekani linatarajiwa kuelezea ripoti kuhusu hali nchini Iraq.Ripoti hiyo inalenga kutoa ufafanuzi kuhusu malengo ya klijeshi na kisiasa ya Marekani tangu uvamizi ulipoanza.

Bunge la Marekani liliagiza hatua hiyo kuchukuliwa ili kutathmini mikakati mipya ya Rais Bush ya kuongeza idadi ya majeshi nchini Iraq.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo bado inasubiriwa baadhi ya malengo yamefikiwa hususan katika usalama ambapo idadi ya vifo vilivyo na misingi ya ghasia za kidini imepungua vilevile mashambulizi ya mabomu.

Hata hivyo ripoti hiyo haitaeleza kuwa uvamizi nchini Iraq haukufaulu.Rais Bush kwa upande wake anashikilia kuwa sharti muda uongezwe ili kujua hali halisi

''Ndio mwanzo tumeanza….hapa Washington baadhi ya watu wanapinga na kusema tuache.Naamini kuwa ni muhimu kwa taifa hili kumpa kamanda huyo mpya nafasi kutekeleza majukumu aliyopewa ndipo bunge litathmini hali halisi kabla kutoa uamuzi wowote.''

Wapinzani wa vita hivyo dhidi ya Iraq katika Bunge la Marekani wanasisitiza kuwa hakuna hatua zozote zilizopigwa tangu majeshi alfu 3 zaidi yalipopelekwa mapema mwaka huu.Nancy Pelosi ni spika wa bunge la Marekani.

''Wanataka vita hivi viishe.Wanataka majeshi yarudi nyumbani.Wanajua kwamba sera tulizofuata nchini Iraq tangu mwanzo hazijafanikiwa.''

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com