WASHINGTON : Urusi yaridhiwa kuwa mwanachama wa WTO | Habari za Ulimwengu | DW | 11.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Urusi yaridhiwa kuwa mwanachama wa WTO

Marekani na Urusi zimefikia makubaliano kimsingi ambapo serikali ya Marekani itaidhinisha kujiunga kwa Urusi katika Shirika la Biashara Duniani WTO.

Maafisa wa Marekani na Urusi wamesema bado ingali kuna mambo yanayohitaji kukamilishwa lakini makubaliano hayo yatatiwa saini kwenye mkutano wa viongozi wa Baraza la Ushirikiano wa Kiuchumi la Asia na Pasifiki utaokafanyika mjini Hanoi nchini Vietnam wiki ijayo.Urusi ni nchi pekee yenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani ambayo hadi sasa sio mwanachama wa shirika hilo.

Kikwazo kikuu katika mazungumzo ya nchi hizo mbili ni suala la nyama ya Marekani kuingizwa Urusi.

Marekani pia imekuwa ikishinikiza sana juu ya suala la kulinda haki miliki na kupatiwa nafasi katika masoko ya huduma za fedha nchini Urusi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com