WASHINGTON : Senate yaunga mkono muswada wa Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 30.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Senate yaunga mkono muswada wa Iraq

Baraza la senate la bunge la Marekani limempa pigo Rais George W. Bush kwa kupitisha muswada ambao utaitaka Ikulu ya Marekani iondowe wanajeshi wa Marekani kutoka Iraq ifikapo mwezi wa Machi mwaka 2008 kama sharti la kuendelea kugharamia zaidi vita nchini Iraq na Afghanistan.

Baraza hilo limepiga kura 51 dhidi ya 47 kuunga mkono muswada huo wa matumizi ya dola bilioni 122 kwa ajili ya vita hivyo na kupuuza tishio kutoka kwa Rais Bush la kuupigia kura ya turufu muswada huo.

Mapema Bush alikutana na wabunge wote wa chama cha Republican kutoka baraza la wawakilishi la bunge la Marekani katika juhudi za kutaka kuungwa mkono kwa msimamo wake.

Baraza hilo wiki iliopita lilipiga kura iliopita chupu chupu kuunga mkono muswada huo ambao umeweka mwezi wa Septemba mwaka 2008 kuwa ni wa mwisho kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka Iraq.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com