WASHINGTON: Gavana wa kimarekani nchini Irak,...
12 Novemba 2003Matangazo
Paul Bremer, ameanza kuzungumza Ikulu baada ya kuwasili ghafula mjini Washington. Hakuna taarifa kamili kuhusika na mkutano wake. Lakini wachambuzi wanasema utawala wake unakatishwa tamaa kwa kutanuka michafuko Irak, na pia udhaifu wa kutenda kazi wa Baraza Tawala la Irak. Bremer alifuta mkutano wake na waziri mkuu wa Poland, Leszek Miller, na akarudi ghafula Ikulu mjini Washington. Katika mazungumzo yake, wamehudhuria pia waziri wa kigeni Colin Powell, mshauri wa masuala ya usalama wa kitaifa Condoleezza Rice, waziri wa ulinzi Donald Rumsfeld na maafisa rasmi wengine muhimu. Ikulu haikusema cho chote madhumuni ya ziara hiyo ya Bremer, wala kama atakutana na rais George W Bush.