WASHINGTON: Bush azungumzia mabadiliko kuhusu mkakati wa Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 12.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Bush azungumzia mabadiliko kuhusu mkakati wa Irak

Marekani inazidi kuashiria kuwa inajitayarisha kufanya mabadiliko makuu katika mkakati wake nchini Irak.Rais George W.Bush,katika hotuba yake ya kila juma kwenye redio amesema,waziri wake mpya wa ulinzi,Robert Gates ni mjumbe wa mabadiliko,atakaeleta mtazamo mpya juu ya njia za kushinda nchini Irak.Bush vile vile ameahidi kushirikiana na Wademokrat ili kuhakikisha ushindi katika vita vya Marekani vya kupambana na ugaidi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com