1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Baraza la Sineta la Marekani limeunga mkono kwa wingi ...

12 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEEF
muswada wa sheria wa kuiwekea vikwazo Syria endapo nchi hii inashindwa, miongoni mwa mambo mengine, kutowaunga mkono wagaidi na kuhamisha askari wake 20 elfu, Libanon. Iwapo haitatekeleza masharti hayo, basi utapunguzwa mno uhusiano wa kiuchumi. Na hata maafisa wa kibalozi wa Syria wataekewa vipingamizi juu ya safari zao nchini Marekani, na pia ndege zake. Inasemekana huenda rais George W Bush akatia sahihi muswada huo. Uhusiano rege-rega baina ya Marekani na Syria tangu vita vya Irak, umezidi kudorora.