Wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wakimbilia nchini Uganda
12 Septemba 2008Matangazo
Wakimbizi hao wanaripotiwa kuingia Uganda kupitia eneo la magharibi la Bunagana na Kisoro linalopakana na Kivu ya kaskazini mashariki mwa Kongo.Mapigano kati ya wanajeshi wa serikali ya Kongo na waasi wanaoongozwa na Laurent Nkunda yalianza mwishoni mwa mwezi Agosti.
Kutoka Kampala Ismail Kigozi anaarifu zaidi