Wahindi wa Uganda wakumbuka siku waliyofukuzwa nchini humo | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.08.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Wahindi wa Uganda wakumbuka siku waliyofukuzwa nchini humo

Kwa muda wa miaka minane kuanzia 1971 hadi 1979, ulidumu utawala wa kutisha nchini Uganda wa Idd Amin Dadah.

default

Rais wa Ujerumani Horst Koehler, katikati ,akitabasam akiwa pamoja na rais wa kilimo nchini Uganda Omara Atubo,wakati alipotembelea nchi hiyo, ambayo hivi sasa imepiga hatua kubwa katika kilimo hasa kwa upande wa kibiashara.

Kwa muda wa miaka nane kuanzia 1971 hadi 1979, ulidumu utawala wa kutisha nchini Uganda wa Idd Amin Dadah. Wakati huo huo katika kipindi hicho watu wanaokadiriwa kufikia laki tano waliuwawa kinyama. Muuaji kutoka Afrika kama alivyofahamika dikteta huyo, aliiharibu nchi hiyo ambayo Winston Churchill aliita kuwa ni lulu ya Afrika na alifahamika kwa kufanya mambo kupita kiasi.

Muda mfupi kabla ya mapinduzi ya kijeshi, ambayo yalimuingiza madarakani , alitangaza mnamo August 4 , 1972 , kuwa watu wenye asili ya Asia wataondolewa kutoka nchini humo.Miaka 30 baada ya Amin , Wahindi wengi bado wanatamani kurudi Uganda. Lakini donda la miaka iliyopita bado halijapona.

Amin aliwapa miezi mitatu. Kila mmoja anaruhusiwa kuchukua masanduku mawili pamoja na paundi 50 fedha za Uingereza. Wengi wa waliofukuzwa walikuwa Wahindi, ambao walifanikiwa sana katika biashara. Mafanikio haya ya kibiashara ndio yaliyosababisha Amin kuchukua hatua hiyo dhidi yao.

Kila wakati dikteta huyo wa Uganda alikuwa akijigamba kuwa Afrika ni kwa Waafrika na Uganda ni kwa ajili ya Waganda tu. Sio Waingereza, ambao ni wakoloni wa zamani wa nchi hiyo ama Wahindi na Waasia, ambao miongo miwili iliyopita ndio walianza kuishi nchini Uganda. Kwa sababu hiyo Amin amezungumzia mengi kuhusu lengo lake. Tarehe 4 August , 1972 Amin alitoa wito. Kwa masikitiko makubwa anakumbuka Mahendra Mehta mwenye umri sasa wa miaka 77 siku hiyo, ambayo alifukuzwa nchini humo.

Huo ulikuwa mwanzo wa maisha mapya. Ilibidi kunza upya kabisa. Na kujaribu kwa kadiri ya uwezo wangu kuisahau Uganda, nchi ambayo ilikuwa ni nyumbani kwangu na kwa muda wa miaka mingi.

Familia ya Mehta iliondoka India mwanzoni mwa karne ya 20 na kwenda kuishi Uganda. Mehta alizaliwa nchini Uganda, akakulia na kuweka mtaji mkubwa katika viwanda na mashamba ya sukari. Mtazamo wa Amini ni kuwa ameinyonya Uganda. Na sio Mehta pekee, lakini hata Wahindi wengine wapatao 90,000 pamoja na watu wengine wenye asili ya Asia, ambao wamekuwa wakiishi Uganda. Mehta ambaye pia amekuwa mbunge, amesalim amri kutokana na woga kuhusiana na mke wake na watoto wawili kuhusiana na nia hiyo ya Amin.

Picha na vitu vichache za ukumbusho, vito, pamoja na sahani ya santuri ambayo aliipenda sana mkewe. Vitu vilivyobakia katika maisha yake. Vitu vingi havikuweza kuingia katika masanduku hayo mawili ambayo ameruhusiwa. Ameondoka na kile ambacho anaweza kubeba mwilini. Tajiri huyo wa viwanda Mehta alikimbilia Canada kama mkimbizi.

Hapa Canada sijisikii vizuri . Utamaduni ni tofauti kabisa, hali ya hewa, watu. Kwa kuwa tayari nilishakuwa Mwaafrika.

Muda mfupi baada ya kuangushwa Amini kutoka madarakani 1980 Mehta alirejea nyumbani, Uganda. Biashara yake hivi sasa ina thamani ya dola milioni 350. Mehta anafanya kila kitu, uzalishaji wa sukari, sementi, mashamba ya maua, vifungashio ama ushauri kwa wafanyabiashara. Kama walivyo wengi wa Wahindi, anasema Maggi Kigozi, mkuu wa ofisi ya uwekezaji nchini Uganda.

Wahindi wanashughulika na mambo mbali mbali. Ikiwa nafasi inajitokeza, wanaikimbilia. Na bila kujali, iwapo shughuli hizo zinafanana ama la. Kwa wakati huu wanajishughulisha zaidi katika nyanja ya nishati, nishati ya sola, nishati inayotokana na maji, gesi inayotokana na vitu hai, lakini pia wanajishughulisha na kilimo.

Rais wa hivi sasa Yoweri Kaguta Museveni hachoki kugusia mara kwa mara kile ambacho Wahindi walichoifanyia nchi ya Uganda. Museveni aliwakaribisha tena Wahindi kurejea nchini humo.

►◄

Mwandishi: Esselborn,Priya/ZR/Sekione Kitojo

Mhariri:Garace Kabogo

 • Tarehe 03.08.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/J2qo
 • Tarehe 03.08.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/J2qo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com