Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanazungumzia hatua ngumu za kuingizwa kwa Uturuki katika umoja wa Ulaya. | Magazetini | DW | 06.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanazungumzia hatua ngumu za kuingizwa kwa Uturuki katika umoja wa Ulaya.

Kutokana na mtazamo ilionao Uturuki kuelekea suala lake na Cyprus , tume ya Ulaya imetoa pendekezo katika mazungumzo ya kujiunga Uturuki katika umoja wa Ulaya . Hii ni mada ambayo imeshughulikiwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo , pamoja na taarifa ya idara ya takwimu inayoelezea idadi mpya wa watu fukara nchini Ujerumani. Pamoja nanyi katika udondozi wa magazeti hii leo ni Sekione Kitojo.

Katika suala la mazungumzo ya kujiunga Uturuki katika umoja wa Ulaya, mhariri wa gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung anaandika:

Kwamba hatua zote za kuingizwa Uturuki katika umoja wa Ulaya ambazo zimechukua zaidi ya mwaka mmoja zimetumbukia katika mzozo.

Ni mzozo ambao unakielelezo kuhusiana zaidi na hatua zilizonyooka za kuingizwa katika umoja wa Ulaya.

Wale walioko Uturuki ambao wanauona Umoja wa Ulaya kama mahali pa kujitajirisha, wanaendeleza mzozo huu na hasimu mkuu wa Uturuki. Wale wenye shaka shaka na Uturuki nao pia hawataki hali hii ibadilike, bali wanataka mzozo huu uendelee, tatizo la Cyprus liendelee kuwapo lakini liwe ndio chanzo.

Kwa mujibu wa wengi wa wanasiasa , wataalamu wa kijamii na kitamaduni hili sio tatizo kubwa, kama inavyoonekana. Kwa hilo wana haki kabisa.

Binafsi iwapo hatua za kuiingiza Uturuki katika umoja wa Ulaya zilizopo zitaendelezwa, zinabaki badala yake kuwa si za kirafiki na kuzidisha machungu.

Mhariri wa gazeti la Nürnberger Zeitung anaelezea moja kwa moja kuhusu mtazamo wa kansela Angela Merkel , ambaye hakuiwekea muda mwingine Uturuki.

Kansela huyo wa Ujerumani ambaye amekosoa sana vipengee kadha vya mapitio , hakua tena anazungumzia hilo jana , baada ya kujenga uelewano na waziri mkuu wa Uturuki na kwamba hatakuwa kizingiti tena dhidi ya njia ya Uturuki kuingia katika umoja wa Ulaya.

Erdohan ni lazima alitambue hilo, na kwa upande wake chama cha SPD kinapaswa kupambana na madai haya ya Angela Merkel.

Maoni ya mhariri wa gazeti la Stuttgater Nachrichten anatoa mtazamo mkali zaidi wa mazungumzo haya kwa kiasi kikubwa kama inavyoonyesha.

Kila wakati mjini Brussels viongozi wanachukulia kwa tahadhari sana linapokuja suala lenye utata na upande wa Waislamu na sio kwa uwazi kamili.

Hapana , hakuna vikwazo katika njia ya Uturuki kuingia katika umoja wa Ulaya, lakini ukweli ni kwamba, nchini Uturuki mtu anatambua ugumu uliopo wa kujiunga. Na kwa hili umoja wa Ulaya binafsi unamakosa.

Mada nyingine iliyoshughulikiwa na wahariri wa magazeti ya leo ni kuhusu watu zaidi ya milioni 10 nchini Ujerumani ambao wanakabiliwa na umasikini. Hii inamaana ya kiasi cha asilimia 13 ya wakaazi wote wa Ujerumani.

Gazeti la Hessische/Niedersächsische Allgemeine kutoka Kassel linatanabahisha kuwa katikati ya majadala huu, kama ilivyo katika suala la wafanyakazi na mapato ya wafanyakazi , taarifa hii inasema, Wajerumani milioni 10 wanaishi karibu na kiwango cha umasikini, na hii ikiwa ni kiasi cha watoto milioni 1.7.

Walioko katika hatari zaidi ni , miongoni mwa kundi la wasio na kazi. Katika nchi hii tajiri, wengi hawawezi kupata kazi, wanakabiliwa na kitisho cha kujihami, kila mmoja ajue mwenyewe jinsi ya kupata fedha. Hii sio njia bora ya kijamii na inatia aibu. Na katika suala la ujinga, mtu anapofikiria kuhusu watoto wote hao , ambao mustakabali wao umepotea kabla ya kuanza. Na kwa hilo kila mmoja anataka ifikapo 2020 nchi hii iweze

kufanyakazi tena kama nchi inayojali masuala ya kijamii.