Wachina katika miji kadhaa ya nchi hiyo waandamana kupinga uhuru wa Tibet | Habari za Ulimwengu | DW | 20.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Wachina katika miji kadhaa ya nchi hiyo waandamana kupinga uhuru wa Tibet

Beijing:

Maandamano ya kupinga uhuru wa jimbo la Tibet yameendelea katika miji kadhaa ya China leo ikiwa ni siku ya pili. Waandamanaji walikusanyika katika duka kubwa la kifaransa mjini Beijing "Carefour" wakipiga kelele kuiunga mkono Jamhuri ya umma wa China na kupinga uhuru wa Tibet.Duka hilo limelengwa kutokana na madai kwamba kampuni ya Carefour ina mafungamano na watibeti wanaoishi uhamishoni, huku kukitolewa wito wa kuzisusia bidhaa zinazotoka Ufaransa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com