1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge wa Marekani wavutana kuhusu matumizi ya serikali

Martin,Prema/dapd,rtre,afpe15 Julai 2011

Waziri wa Fedha wa Marekani Timothy Geithner ametoa mwito wa dharura kwa wabunge kukubaliana kiwango cha juu cha deni la taifa.

https://p.dw.com/p/RZw3
United States Secretary of the Treasury Timothy Geithner speaks during a session at the World Economic Forum in Davos, Switzerland on Friday, Jan. 28, 2011. In a nod to the post-crisis atmosphere, the World Economic Forum shifts its attention on Friday to austerity measures and priorities for improving the economy. (Foto:Michel Euler/AP/dapd)
Waziri wa Fedha wa Marekani, Timothy GeithnerPicha: dapd

Geithner amewaambia wabunge wa vyama vya Demokratik na Republikan kuwa ulimwengu unapaswa kupewa ishara moja kwa moja, kuwa Marekani inaweza kutekeleza wajibu wake wa kulipa madeni.

Mwenyekiti wa Benki Kuu ya Marekani, Ben Bernanke pia, ameonya kuwa hatua ya kupunguza matumizi ya serikali kwa kiwango kikubwa, huenda ikazuia ukuaji wa kiuchumi ulio dhaifu na hivyo kuathiri uchumi wa Marekani na ulimwengu mzima.

Der Praesident der US-amerikanischen Notenbank, Ben Bernanke, spricht am Freitag (19.11.10) in Frankfurt am Main auf einer Konferenz der Europaeischen Zentralbank (EZB). Die aktuelle Geldmarktpolitik und Lehren aus der Finanzkrise standen im Fokus der zum 6. Mal statfindenen Veranstaltung. Foto: Mario Vedder/dapd
Mwenyekiti wa Benki Kuu ya Marekani, Ben BernankePicha: dapd

Shirika la Moody's linalotathmini uwezo wa taifa kulipa mikopo, limeonya kuishusha Marekani katika tabaka la chini kwa sababu ya majadiliano ya bajeti kutosonga mbele. Hata shirika la China, Dagong limeeleza fikra kama hiyo.