Waasi wa Kihutu wailaumu Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 15.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Waasi wa Kihutu wailaumu Marekani

NAIROBI.Waasi wa Rwanda wa Kihutu, ambao wamekimbilia katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wameishutumu Marekani kwa kumsaidia Jeneral muhasi Laurent Nkunda huko mashariki wa kongo.

Katika taarifa yao iliyopatikana jijini Nairobi , waasi hao wa Democratic Forces for the Liberation of Rwanda FDLR wameserma kuwa jeshi la Marekani limekuwa likitoa misaada mbali kwa Jenerali Nkunda.

Wamesema kuwa askari wa Marekani wameweka kambi katika mji wa mpakani wa Gisenyi ambako wanatoa misaada ya kivita ikiwemo silaha, taarifa za kijasusi na ulinzi binafsi kwa Jenerali Nkunda.

Nkunda amekuwa akidai kuwa anapigana kuwalinda watu wa kabila lake ambao ni wakongo wenye asili ya kitutsi dhidi ya waasi hao wa FDLR.

Wakati huo huo Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UHCR Antonio Guterres yukoa katika ziara ya eneo la Mashariki mwa Kongo ambako maelfu kadhaa ya watu wamekimbia mapigano.

Mapigano hayo ni kati ya majeshi ya Serikali na ya Jenerali huyo muasi Laurent Nkunda

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com