1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Viongozi wa Ulaya walaani vikali tangazo la ushuru la Trump

18 Januari 2026

Nchi za Ulaya zinazolengwa na ushuru uliotangazwa na Rais Donald Trump katika kauli ya pamoja zimesema Jumapili 18.01.2026 zitaendelea kusimama pamoja na kushirikiana katika kujibu vitisho vya Marekani.

https://p.dw.com/p/570x7
Brüssels, Ubelgiji 2025
Viongozi wa mataifa ya Ulaya wamekosoa tangazo la Trump la kuziwekea ushuru nchi 8 zinazopinga azma yake ya kuinunua GreenlandPicha: Stephanie Lecocq/REUTERS

Mataifa ya Denmark, Norway, Sweden, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi na Uingereza yameonya kuwa vitisho hivyo vya ushuru vinakwamisha ushirikiano kati ya Ulaya na Marekani.

Awali, Trump alitangaza kuziwekea ushuru wa asilimia 10 nchi hizo zinazopinga juhudi zake za kukinunua kisiwa cha Greenland. Amesema ushuru huo utaendelea hadi mpango wa kuinunua Greenland utakapofanikiwa na huenda ukatekelezwa mpaka Juni 25 kama hakutafikiwa makubaliano.

Viongozi wa Ulaya wasema kitisho cha ushuru ni kosa kubwa

Kabla ya kauli hiyo ya pamoja Waziri Mkuu wa Italia mwenye uhusiano mzuri na Trump aliiionya hatua hiyo ya Trump aliyoitaja kuwa kosa kubwa. Naye msaidizi wa Kansela wa Ujerumani ambaye pia ni Waziri wa fedha Lars Klingbeil amesema Ujerumani na washirika wake wa Ulaya hawatakubali kushurutiswa na Marekani.