EU yajiandaa kwa jibu la pamoja dhidi ya ushuru wa Trump
18 Januari 2026
Matangazo
Nchi hizo ni zile zinazopinga juhudi za Trump za kuinunua Greenland. Alitangaza kuwa ushuru huo utaendelea hadi mpango wa kuinunua Greenland utakapofanikiwa na huenda ushuru huo ukatekelezwa mpaka Juni 25 kama hakuna makubaliano yatakayofikiwa.
Juhudi za kuzuia ushuru wa Trump zaendelea
Wakati huohuo, kiongozi wa walio wachache wa chama cha Democratic katika baraza la Seneti la Marekani, Chuck Schumer ameahidi kufanya juhudi za kuzuia ushuru aliotishia kuuweka Rais Trump dhidi ya washirika wa Ulaya kutokana na mzozo wa Greenland.
Katika taarifa yake iliyotolewa Jumamosi, Schumer amesema ushuru unaotangazwa na Trump wa kukurupuka umeshasababisha mfumuko mkubwa wa bei na kuuharibu uchumi wa Marekani.