1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaDenmark

Vikosi kutoka nchi za Ulaya vyaendelea kuwasili Greenland

16 Januari 2026

Vikosi vya wanajeshi kutoka nchi kadhaa za Ulaya ikiwemo Ujerumani na Ufaransa, vinaendelea kuwasili katika kisiwa kinachojitawala cha Greenland ili kuonyesha uungaji mkono kwa Denmark.

https://p.dw.com/p/56ueQ
Nuuk | Wanawake wakisimama karibu na bendera ya kisiwa cha Greenland
Wanawake wakisimama karibu na bendera ya kisiwa kinachojitawala cha Greenland katika mji wa Nuuk.Picha: Evgeniy Maloletka/AP Photo/picture alliance

Hii ni baada ya mazungumzo kati ya Marekani na wawakilishi wa Denmark na Greenland  kushindwa kufikia muafaka kuhusu mustakabali wa kisiwa hicho cha Aktiki.

Ikulu ya White House imesisitiza kuwa kitakachofuata kwa sasa ni "mazungumzo ya kiufundi" kuhusu makubaliano yatakayoiwezesha Marekani kuinunua  Greenland.

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Lars Løkke Rasmussen amekanusha kauli hiyo na kusema kumeundwa timu itakayojadili namna ya kutatua tofauti zilizopo kati ya mataifa hayo.