Uongozi wa kijeshi Misri walivunja bunge | Matukio ya Kisiasa | DW | 14.02.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Uongozi wa kijeshi Misri walivunja bunge

Uongozi mpya wa kijeshi nchini Misri umetangaza kulivunja bunge na kusimamisha katiba, siku mbili baada ya kujiuzulu rais wa nchi hiyo, Hosni Mubarak.

default

Kiongozi wa kijeshi Misri, Field Marshal Mohammed Hussein Tantawi

Katika taarifa yake, Baraza Kuu la Kijeshi jana lilisema kuwa litasimamia masuala ya nchi hiyo hadi uchaguzi mpya wa wabunge utakapofanyika.

Serikali hiyo mpya ya Misri pia ilikutana kwa mara ya kwanza, ikisema kuwa kipaumbele chake cha kwanza ni kurejesha hali ya usalama na kuwezesha maisha ya kila siku ya raia wake.

Waziri Mkuu, Ahmed Shafiq amesema hana haraka ya kuwateua mawaziri, na badala yake atafanya tu maamuzi iwapo ana imani ya kutosha katika uteuzi.

Pia Waziri huyo Mkuu wa Misri, alisema serikali itaweka kipaumbele katika kupunguza bei za vyakula, wakati ambapo mamilioni ya Wamisri wanategemea ruzuku ya serikali ili kuishi.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com