1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kuekeza zaidi eneo la Arctic

23 Januari 2026

Umoja wa Ulaya haujaekeza vya kutosha kwa usalama wa eneo la Arctic na sasa ndio wakati wa kubadilisha hilo na kuekeza zaidi.

https://p.dw.com/p/57GiZ
Rais wa Halmshauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen
Rais wa Halmshauri Kuu ya Ulaya Ursula von der LeyenPicha: Nicolas Tucat/AFP

Haya yamesemwa na Rais wa Halmshauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula vonder Leyen. Akizungumza mjini Brussels, Von der Leyen amesema Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya hivi karibuni itapendekeza kitita kikubwa cha uwekezaji kwa Greenland, eneo la Denmark lililo na utawala wa ndani.

Mkuu huyo wa Umoja wa Ulaya ameyasema haya leo kufuatia mkutano wa kilele wa viongozi wa umoja huo ambapo walikuwa wanakutana baada ya mahusiano yao na Marekani kutikiswa na kitisho cha Rais Donald Trump cha kuyawekea mataifa kadhaa ya Ulaya ushuru katika bidhaa zake, kwa kukiunga mkono Denmark katika azma yake ya kuzuia kutwaliwa kwa Greenland na Marekani.

Wakati huo huo Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa amesema kuwa umoja huo utaendelea kujilinda kutokana na ukandamizaji au shinikizo la aina yoyote ile.