Umoja wa Mataifa watoa onyo kwa Rais Gbagbo. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 18.12.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Umoja wa Mataifa watoa onyo kwa Rais Gbagbo.

Shinikizo dhidi ya Laurent Gbagbo kuendelezwa.

default

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemwonya Gbagbo dhidi ya kuzuia kazi za Umoja huo nchini Ivory Coast.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameionya serikali ya Ivory Coast dhidi ya kuuzuia Umoja wa Umoja wa Mataifa kufanya kazi zake nchini humo. Katibu Mkuu Ban amesema hali imegeuka kuwa ya hatari nchini Ivory Coast.

Amesema jaribio lolote la kuzuia kazi za Umoja wa Mataifa halitakubalika. Katibu mkuu huyo kwa mara nyingine amemtaka rais Laurent Gbagbo ajiuzulu na akubali kwamba kiongozi wa upinzani, Alassane Outtara ndiye alieshinda uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita na kuthibitishwa na Umoja wa Mataifa.

Hapo awali viongozi wa Umoja wa Ulaya walitishia kuweka vikwazo vya kiuchumi na wamempa rais Gbagbo muda wa hadi mwishoni wiki ili ajiuzulu.Habari zaidi zinasema jumuiya ya kimataifa inatayarisha vikwazo vya fedha ili kumlazimisha Gbago ajiuzulu.Wataalamu wamesema kuwa vikwazo hivyo vitaelekezwa katika akiba ya za benki.Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa bibi Michele Alliot-Marie amesema kuwa ni lazima kuendeleza shinikizo dhidi ya rais Gbagbo

 • Tarehe 18.12.2010
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Qf8W
 • Tarehe 18.12.2010
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Qf8W

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com