1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatoa uchunguzi wa awali wa mazungumzo yaliovuja

Sylvia Mwehozi
5 Machi 2024

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amewasilisha matokeo ya awali ya uchunguzi kuhusu kuvuja kwa mazungumzo ya maafisa waandamizi wa kijeshi wa Ujerumani juu ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4dCQV
Ujerumani Berlin | Mkutano na waandishi wa habari Waziri wa Ulinzi Boris Pistorius juu ya upigaji simu
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius akizungumza na vyombo vya habari kufuatia ufichuzi wa hivi majuzi kwamba idara za ujasusi za Urusi zilisikiliza simu kati ya maafisa wa ngazi za juu wa Ujerumani, Machi 05, 2024 huko Berlin, Ujerumani.Picha: Maja Hitij/Getty Images

Pistorius amesema mshiriki mmoja katika mazungumzo hayo, yaliyodukuliwa na Urusi, kwa bahati mbaya alijiunga kwa kutumia laini isiyo salama. Waziri huyo ameeleza kuwa Urusi, huenda iliingilia mazungumzo kati ya maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi la anga la Ujerumani kwa bahati mbaya kupitia uchunguzi ulioenea. Vyombo vya habari vya Urusi wiki iliyopita, vilichapisha mkanda wa sauti wa mkutano wa maafisa wa Ujerumani uliofanyika katika jukwaa la Webex, wakizungumzia upelekaji wa silaha huko Ukraine na uwezekano wa shambulizi la Kiev kwenye daraja huko Crimea. Kuvuja kwa mazungumzo hayo kumeiabisha Ujerumani na kuzua maswali juu ya usalama wake wa kijasusi.