1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yakanusha ajenda ya kisasi kwa kuisaidia Ukraine

3 Februari 2026

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani, Johan Wadephul, amekanusha tuhuma za Urusi kwamba uungaji mkono wa nchi yake kwa Ukraine unatokana na kisasi kutokana na kushindwa utawala wa Kinazi kwenye Vita vya Pili vya Dunia.

https://p.dw.com/p/57xCq
Johan Wadephul
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani, Johan Wadephul, anasema nchi yake haikwepi ukweli wa kihistoria kwenye kuisaidia Ukraine dhidi ya Urusi.Picha: Simon Wohlfahrt/AFP/Getty Images

Akizungumza wakati wa mkutano na mwenzake wa New Zealand, Winston Peters, Wadephul alisema Ujerumani haina tatizo na kukubaliana na ukweli na jukumu la Muungano wa Kisovieti kwenye kuushinda utawala wa Kinazi wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.

Urusi ilisema hapo awali kwamba sera ya nje ya Ujerumani kuelekea Ukraine inaundwa na dhana ya ulipizaji kisasi, ikiituhumu Berlin kwa kuishi na andasa za kurekebisha mambo iliyoyapoteza kwenye historia yake.

Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wa kila mwaka wa waandishi wa habari wa Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov, Urusi ilisema uungaji mkono usio masharti kwa Ukraine una ajenda ya kulipiza.