Ujerumani kupambana na Marekani katika nusu fainali | Michezo | DW | 29.06.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ujerumani kupambana na Marekani katika nusu fainali

Michuano ya nusu fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake inatarajiwa kuwa na msisimko wa na burudani la aina yake, kwa kuwaleta miamba watatu wa mchezo huo pamoja na England

Mjini Montreal hapo kesho Jumanne, Ujerumani, mabingwa wa mwaka wa 2003 na 2007, watashuka dimbani na Marekani, waliotwaa Kombe hilo mwaka wa 1991 na 1999, na pia washindi mara tatu mfululizo wa medali za dhahabu katika Michezo ya Olimpiki.

Ujerumani iliizidi nguvu Ufaransa iliyojikakamua kwelikweli, kupitia mikwaju ya penalti, na sifa yake ya kandanda la kasi na la mashambulizi inatarajiwa kudhihirika wakati wanawake hao watakapokutana na timu ya Marekani yenye wachezaji wenye vipaji ambayo iliipiku China goli moja kwa sifuri.

Licha ya matokeo bora ambayo Wajerumani wamepata, mlinda mlango wa Marekani Hope Solo anaamini wajerumani watalazimika kuimarika ikiwa wangetaja kuwapiku Wamarekani.

Marekani imeendeleza rekodi yake ya kutinga nusu fainali ya kila Dimba la Kombe la Dunia na wachezaji wa timu ya taifa wanaamini kuwa mchango wa mashabiki wao umekuwa mkubwa katika mafanikio yao ya sasa. Amy Rodriguez ni mshambuliaji wa timu ya Marekani

Mchuano huo wa kesho utakuwa marudio ya nusu fainali ya mwaka wa 2003, ambayo Ujerumani iliishinda Marekani nyumbani kwao magoli matatu kwa bila.

Japan dhidi ya England

Nusu fainali ya pili itachezwa Jumatano mjini Edmonton, wakati mabingwa watetezi wa ulimwengu Japan wakikutana na timu ya England ambayo iliwanyamazisha wenyeji wa michuano ya mwaka huu Canada, na kutinga nne bora kwa mara ya kwanza katika historia.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Rueters
Mhariri:Iddi Ssessanga