Uganda yawarefushia muda waasi wa LRA | Habari za Ulimwengu | DW | 30.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Uganda yawarefushia muda waasi wa LRA

Uganda imewarefushia muda waasi wa kundi la Lords Resistance Army, LRA, kusaini mkataba wa amani.

Hatua hiyo inapunguza uwezekano wa harakati ya jeshi la Uganda dhidi ya kundi hilo la waasi kutokea hivi karibuni.

Serikali ya rais Yoweri Museveni ilimpa kiongozi wa kundi la LRA, Joseph Kony, hadi mwisho wa mwezi huu asaini mkataba wa amani au akabiliwe na kitisho cha kurudi katika vita.

Mazungumzo ya amani yanatarajiwa kuanza tena hii leo. Kiongozi wa ujumbe wa Uganda katika mazungumzo ya amani yaliyoanza mwaka jana mjini Juba huko Sudan Kusini, na ambaye pia ni waziri wa mambo ya ndani wa Uganda, Ruhakana Rugunda, amesema kurefushwa kwa muda huo kunatoa nafasi mazungumzo yafanyike katika hali nzuri itakayowezesha makubaliano yasainiwe hivi karibuni.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com