1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa na Marekani zaandaa azio la kukabiliana na uharamia Somalia

23 Aprili 2008

-

https://p.dw.com/p/Dn0y

NEW-YORK

Ufaransa na Marekani zikisaidiwa na Uingereza zinaandaa azimio la Umoja wa mataifa litakalozipa uwezo nchi kupambana na uharamia katika pwani ya Somalia na maeneo mengine.Taarifa hizo zimetolewa na balozi wa Ufaransa katika Umoja wa mataifa ambaye amesema wako katika hatua za kukubaliana miongoni mwao juu ya kitakachokuwemo ndani ya azimio hilo ikiwa ni pamoja na masuala ya kisheria. Kuongezeka kwa visa vya utekaji nyara katika pwani ya Somalia vinavyofanywa na maharamia kumelifanya eneo hilo kuwa hatari kabisa kwa meli zinazopitia bahari hiyo.Jumatatu maharamia wakisomali waliiteka nyara meli iliyokuwa inaelekea Dubai na Uhispania imesema imepeleka meli ya kijeshi baada ya kutekwa nyara kwa boti la uvuvi la nchi yake likiwa na wafanyikazi 26.Duru za kibalozi zinasema azimio hilo la pamoja huenda likataka kuwepo kwa Umoja wa mataifa nchini Somalia taifa ambalo nchi nyingi bado zinakataa kutuma majeshi yake kuweka amani.