1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump azungumza na Merz, Takaichi baada ya kuondoka China

15 Mei 2026

Rais Donald Trump wa Marekani amefanya mazungumzo kwa njia ya simu leo na washirika wake kadhaa akiwa njiani kurejea nyumbani baada ya kukamilisha ziara yake nchini China aloitaja kuwa ya "mafanikio makubwa."

https://p.dw.com/p/5Dopt
China Beijing 2026 | Rais Donald Trump wa Marekani akiabiri ndege ya Air Force One
Rais Donald Trump wa Marekani akiondoka Beijing, China. Picha: Mark Schiefelbein/AP Photo/picture alliance

Trump kwanza alizungumza na Kansela Friedrich Merz wa Ujerumani na kwa pamoja wamesisitiza msimamo wao wa kutaka kuizuia Iran kumiliki silaha za nyuklia na haja ya kufunguliwa kikamilifu kwa Mlango Bahari wa Hormuz.

Mazungumzo mengine ameyafanya na Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi yaliyojikita juu ya masuala kuhusu China hasa baada ya ziara ya siku tatu ya Trump mjini Beijing alikokutana na Rais Xi Jinpinga.

Mbali ya mazungumzo hayo, Trump amewaambia waandishi habari akiwa kwenye ndege ya Air Force One kuwa ziara yake ya China imefanikisha" kutiwa saini mikataba mizuri ya biashara" na "kutatua changamoto nyingi baina ya pande hizo mbili"