TRIPOLI: Nchi za Ulaya na Afrika zazungumzia swala la uhamiaji
23 Novemba 2006Matangazo
Wajumbe kutoka nchi zaidi ya 50 za Umoja wa Ulaya na mataifa ya kiafrika, wameanza jana mkutano wa siku mbili katika mji mkuu wa Libya Tripoli. Mkutano huo utajadili maswala ya uhamiaji.
Huo ni mkutano wa kwanza wa aina yake unaotarajiwa kuzingatia maswala ya uhamiaji haramu, uhamiaji halali na sheria zinazowalinda wakimbizi. Mkutano huo unafanyika wakati wimbi kubwa la wahamiaji hasa kutoka bara la Afrika, wanajaribu kuingia barani Ulaya katika harakati za kuukimbia umasikini uliko katika nchi zao.
Ma mia ya wakimbizi hao wamezama au kufa kwa njaa katika safari zao baharini wakitumia maboti.