TEL AVIV: Israil yakanusha tetesi za vita kati yake na Syria. | Habari za Ulimwengu | DW | 07.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEL AVIV: Israil yakanusha tetesi za vita kati yake na Syria.

Waziri Mkuu wa Israil, Ehud Olmert, amekanusha uvumi kwamba huenda nchi hiyo ikaingia vitani na Syria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wa kiusalama kujadili suala hilo, waziri mkuu huyo amesema anazingatia sana amani kati ya nchi yake na Syria.

Hata hivyo amesema tukio lolote lisiloelekea huenda likasababisha makabiliano kati ya mataifa hayo mawili.

Vyombo vya habari nchini Israil vimekuwa vikitoa habari kwamba huenda vita vikazuka kati ya mataifa hayo mawili kutokana na taarifa za kijasusi zilizodai Syria inajiandaa kwa vita.

Majeshi ya Israil siku ya jumanne yalianza mazoezi ya kijeshi ambapo yalikishambulia pia kijiji kimoja nchini Syria.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com