Tanzania: Polisi wavamia nyumba na ofisi za mhariri wa gazeti la Mwanahalisi
21 Julai 2008Matangazo
Kwa mujibu wa taarifa tulizopokea maafisa hao walinakili maelezo yaliyokuwa kwenye komputa binafsi ya Bwana Kubenea ila hawakumuonyesha maelezo yaliyokuwamo kwenye vifaa walivyotumia kunakili.Itakumbukwa kuwa Saidi Kubenea alimwagiwa tindi kali miezi michache iliyopita alipovamiwa na watu wasiojulikana akiwa afisini mwake.
Mwandishi wetu wa Dar es salaam Christopher Buke amezungumza na mhariri huyo wa gazeti la Mwanahalisi Said Kubenea.