Tanzania: Chiligati azungumza juu ya kashfa za rushwa na Muwafaka wa Zanzibar
30 Septemba 2008Kwa mwaliko wa Wakfu wa Friedrich Ebert ulio karibu na Chama cha Social Democratic, SPD, hapa Ujerumani, katibu wa itikadi wa Chama tawala cha CCM nchini Tanzania, John Zephania Chiligati, ambaye pia ni waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makaazi, amekuweko hapa Ujerumani kwa wiki nzima. Vyama vya SPD na CCM vina urafiki na ushirika wa miaka mingi tangu zama za viongozi wa vyama hivyo, marehemu Willy Brandt na Mwalimu Julius Nyerere. Alipolitembelea jengo letu la Deutsche Welle, nilipata nafasi ya kuzungumza naye, na kwanza niltaka kujuwa zaidi kutoka kwake juu ya madai ya kashfa za rushwa ambazo zimewakumba viongozi kadhaa wa chama na serekali huko Tanzania, jambo ambalo wachunguzi wanasema limekipunguzia umaarufu chama cha CCM....