SPRINGFIELD : Obama kuwania urais wa Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 11.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SPRINGFIELD : Obama kuwania urais wa Marekani

Seneta wa chama cha Demokrat Barack Obama ametangaza rasmi nia yake ya kuwania Urais wa Marekani katika uchaguzi uliopangwa kufanyika hapo mwaka 2008.

Obama anawania kuwa rais wa kwanza mweusi nchini Marekani.Amewahutubia wafuasi wake huko Sprigfield mji mkuu wa jimbo la Illinois mahala ambapo Abraham Lincoln alitowa wito wa kukomeshwa kwa utumwa nchini Marekani.Obama ameahidi kuongoza kizazi kipya ambacho kitajenga Marekani yenye matumaini makubwa zaidi.Katika suala la Iraq amesema wakati umefika kwa wanajeshi wa Marekani kurudi nyumbani.

Obama anaonekana kuwa miongoni mwa masenata mashuhuri wa chama cha Demokrat wanaowania kuingia Ikulu ya Marekani akiwemo seneta Hilary Clinton mke wa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com