Spika mpya wa bunge aeleza ajenda ya Warepublikan | Matukio ya Kisiasa | DW | 06.01.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Spika mpya wa bunge aeleza ajenda ya Warepublikan

Bunge jipya la Marekani limekutana kwa mara ya kwanza,kufuatia uchaguzi uliofanyika mwezi wa Novemba.

### House speaker-in-waiting Rep. John Boehner, R-Ohio, gestures during a news conference on Capitol Hill in Washington, Wednesday, Nov. 3, 2010. (AP Photo/Alex Brandon)

John Boehner,spika mpya wa bunge la Marekani.

Baada ya kushinda uchaguzi huo, chama cha Republikan kinadhibiti baraza la waakilishi bungeni, wakati chama cha Demokratik cha Rais Barack Obama kikibakia na uwingi mdogo katika Seneti.

John Boehner alieteuliwa spika mpya wa bunge,amemrithi Nancy Pelosi wa chama cha Demokratik. Katika hotuba yake,spika huyo mpya ametangaza mpango wa kupunguza matumizi ya serikali, kwa kiasi cha dola bilioni 100 kila mwaka. Lengo ni kupunguza nakisi ya dola trilioni 1.3 katika bajeti ya nchi hiyo. Chama cha Republikan kinataka pia kubatilisha mageuzi muhimu yaliyofanywa na Rais Obama katika huduma za afya,lakini chama cha Demokratik kinaweza kuizuia ajenda hiyo ya Warepublikan.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com