Serbia yapanga kuzipinga Eu na Marekani | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 25.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Serbia yapanga kuzipinga Eu na Marekani

---

BELGRADE

Serbia inapanga kuidhinisha hapo kesho hatua za kuyapinga mataifa ya Magharibi ikiwa yatatangaza uhuru kwa jimbo la Kosovo.Hatua hizo ni pamoja na kuzuia jeshi la Umoja wa Ulaya katika jimbo la Kosovo na kuvunja uhusiano na nchi za Umoja huo pamoja na Marekani.Bunge la Serbia kesho litajadili juu ya azimio kali lililopendekezwa na serikali ambalo linawataka maafisa wote wa nchi hiyo kukataa kabisa uhuru wa jimbo la Kosovo.Waalbania katika jimbo hilo wameapa kujitangazia uhuru mapema mwaka ujao.Marekani na nchi nyingi za Ulaya zimeashiria kukubaliana na suala hilo.Serbia ikiungwa mkono na mshirika wake Urussi zinapinga kabisa hatua hiyo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com